Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza Kulia) akielekea kupanda Boti ya
kumpeleka Musoma Mjini mara baada ya kuzindua Mpango
wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo uliofanyika katika shule ya
Rukuba iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ambayo ilipata madawati 100 huku
zoezi hilo likiwa ni endelevu. Wa Pili kutoka kulia ni Mhandisi Joseph
Kumburu.
Walimu
wa Shule ya Msingi Rukuba katika Jimbo la Musoma Vijijini wakiwa
wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya
kuzindua Mpango
wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika
kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni
endelevu.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Rukuba katika Jimbo la Musoma Vijijini wakiwa
wamekalia madawati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya
kuzindua Mpango
wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika
kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni
endelevu.
Wananchi
wa Kijiji cha Saragana katika Jimbo la Musoma Vijijini (kushoto)
wakifuatilia uzinduzi Tovuti ya Jimbo ambapo wadau mbalimbali wa ndani
na nje nchi watapata taarifa mbalimbali kuhusu Jimbo hilo. Uzinduzi wa
Tovuti hiyo ulifanywa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo
pichani).
Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ( wa Pili kushoto) akipeana mkono na mmoja wa
Wanafunzi katika Shule ya Msingi Rukuba iliyopo jimboni humo ikiwa ni
ishara ya uzinduzi wa Mpango
wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika
kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni
endelevu.
MBUNGE
wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo amezindua Tovuti ya Jimbo la Musoma Vijijini
ambapo wadau mbalimbali wa ndani na nje nchi watapata taarifa mbalimbali
kuhusu Jimbo hilo.
Uzinduzi
wa Tovuti hiyo ulifanyika katika Kijiji cha Saragana wilayani Musoma
ambapo wananchi mbalimbali na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya
Musoma Vijijini walihudhuria.
“Badala
ya kusubiri kuangalia Luninga au magazeti, Tovuti hii itasaidia
shughuli mbalimbali za Jimbo ikiwemo miradi mbalimbali tunayotekeleza
kuonekana katika ulimwengu mzima”, alisema Profesa Muhongo.
Aidha
alisema kuwa Tovuti hiyo inarahisisha Mawasiliano kati ya Mbunge na
wananchi wa Jimbo hilo kwani sasa wataweza kuuliza maswali au kutoa
maoni yao moja kwa moja kuhusu jimbo husika.
Aliongeza
kuwa kuonekana kwa miradi inayotekelezwa jimboni humo, ikiwemo ya
Afya, Elimu, na Kilimo kutasaidia kuvutia wafadhili mbalimbali
kuendeleza miradi husika, akitolea mfano zoezi la uchangiaji fedha za
kutengeneza madawati linaloendelea sasa ambalo litawezesha madawati 8000
kutengenezwa.
Awali
Profesa Muhongo alizindua pia Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo
hilo la Musoma Vijijini ambapo alizindulia mpango huo katika shule ya
msingi Rukuba iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ambayo ilipata madawati
100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.
Alisema
kuwa Jimbo hilo lina upungufu wa madawati 8000 hivyo utengenezaji wa
madawati hayo unaendelea kupitia SUMA-JKT mkoani Mwanza na kwamba fedha
za kutengenezea madawati zimetoka kkwa Mbunge huyo pamoja na wadau
mbalimbali walioguswa na tatizo hilo.
“
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ndani ya miezi mitatu ijayo kuwe hakuna
mtoto anayekaa chini katika shule za msingi zote 108 zilizopo jimboni
humu, na fedha hizi za utengenezaji madawati hutumwa moja kwa moja
kwenye akanti ya iliyotolewa na SUMA JKT, hii yote ni katika kuhakikisha
kuwa zoezi hili linafanyika kwa ufanisi,” alisema Profesa Muhongo.