Wakurugenzi, Waganga Wakuu itangazeni NHIF- Waziri Jaffo

April 16, 2016

NH1 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jaffo akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa kupokea msaada wa Magodoro 60 kutoka NHIF, kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo na kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko NHIF.
NH2 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo akiongozana na Naibu Waziri (TAMISEMI) Seleman Jaffo wakati wa kupokea msaada kutoka NHIF.
NH3Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani akitoa maelezo ya awali juu ya misaada ambayo Mfuko umetoa katika maeneo mbalimbali.
NH4 
Naibu Waziri Mh Suleiman Jafo akipata maelezo wodini kutoka kwa mganga mkuu wahospitali  ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo
NH5 
Naibu Waziri Suleiman Jaffo akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Msoko NHIF Bw. Rehani Athumani.
NH6 
Naibu Waziri Suleiman Jaffo akisikiliza jambo kutoka kwa Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Michael kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko Bw. Rehani Athumani.
NH7 
Naibu Waziri Suleiman Jafo akielezea mikakati ya Serikali ya awamu ya tano katika uboreshaji wa huduma.
NH8 
Magodoro yakishushwa tayari kwa kupokelewa.
NH9
NH10 
Kazi ikiendelea.
……………………………………………………………………………………………………
Na Grace Michael
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya umuhimu na matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watumishi wengine ili waweze kunufaika na huduma hizo.
Mbali na hilo, ameupongeza Mfuko huo kwa jitihada ambazo umekuwa ukifanya katika kushughulikia changamoto mbalimbali hususan za huduma za matibabu katika maeneo yote wanapokutana nazo.
Hayo ameyasema wilayani Kisarawe wakati akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka NHIF ambao ambao umekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kusambazwa katika vituo vya afya ambavyo vina uhitaji mkubwa.
“Katika hili NHIF mmefanya vizuri sana ….na sio hapa tu, nimekuwa nikipita katika maeneo mbalimbali na taarifa zenu nakutana nazo kuwa mmekuwa wepesi sana katika kushughulikia matatizo hasa ya uboreshaji wa huduma za afya pale mnapokutana nayo,”
“Mmeboresha sana huduma zenu kwa wanachama wenu hasa kwa kupanua wigo wa vituo vya kutolea huduma hatua inayowawezesha wanachama kupata huduma mahali popote wanapotaka wao…sasa naomba viongozi wa halmashauri hakikisheni mnawapa elimu watumishi na wananchi kwa ujumla juu ya huduma hizi za Mfuko,” alisisitiza Naibu Waziri Jaffo.
Akitoa maelekezo ya mgao wa magodoro hayo, alimtaka Mganga Mkuu kutoa kipaumbele katika Vituo vya Afya vya Mwanerumango, Masaki na Mzenga kwa kuwa vina uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.
Kwa upande wa NHIF, akikabidhi magodoro hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani alisema kuwa Mfuko ulibaini changamoto ya ukosefu wa magodoro wilayani humo wakati ilipopita kwa ajili ya ugawaji mashuka hivyo Mfuko ulidhamiria kuondoa tatizo hilo.
“Tulipita katika vituo mbalimbali wilayani hapa wakati tunagawa mashuka siku ya sherehe za Uhuru ambapo Mfuko pia ulishiriki katika kufanya usafi katika vituo hivyo…baada ya kuona tatizo hilo Uongozi wa Mfuko uliona kuna haja kubwa ya kubana matumizi katika maeneo mengine kwa lengo la kuwasaidia wananchi,” alisema Bw. Rehani.
Alisema kuwa jitihada za kubana matumizi zimeuwezesha Mfuko kutoa misaada ya Magodoro 60 wilayani Kisarawe, mabati 400 katika zahanati ya Mpingi, Songea Vijijini, Vitanda 20 na magodoro 20 katika kituo cha afya cha Mjimwema mkoani Ruvuma pamoja na saruji tani tatu katika Shule ya Sekondari ya Kilangalanga.
“Mfuko huu ni wa Watanzania wote sisi tumepewa dhamana ya kuusimamia hivyo ni lazima twende na kasi ambayo Rais wetu anaitaka kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na niseme tu kwamba Huduma bora za Afya Tanzania inawezekana.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »