Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za
rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia
kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa
FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.
Katika salamu zake, TFF imewapa pole familia ya marehemu Ngofilo
ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu kanda ya Ziwa na kusema
Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hiki cha maomblezo.
Mazishi ya Silvanus Makalu Ngofilo yatafanyika kesho Jumapili
kijijini kwao Mwamanyili, Wilayani ya Busega mkoa wa Shinyanga ambapo
TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedasto Lufano.
Marehemu Ngofilo wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti
wa FAT wakati wa Muhidin Ndolanga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
FAT, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA)
1984-1994, ambapo baada ya kustaafu alipewa wenyekiti wa heshima na
MZFA.