Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka jipya la kisasa jijini Mwanza ndani ya Mwanza Rock City shopping Mall litakalowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel wakati wowote wakiwa wanafanya manunuzi mbalimbali katika Mall hiyo
Duka
hilo la jipya la Airtel Rock City Shop ni duka la tatu kuzinduliwa kwa
mwaka huu kwa lengo la kuendelea kukamilisha dhamira ya Airtel ya
kuongeza vituo vya kutoa huduma bora kwa wateja wake wanaoongezeka kila
siku nchi nzima.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa duka hilo , Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja, Bi Adrian Lyamba alisema” Duka hili tunalozindua leo litaweza
kuwahudumia wateja kutoka katika maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa
watakaokuja kutembelea Rock City Mall kwa mahitaji mengine. kupitia
duka hili pia tunawahakikishia wateja wetu usalama wa pesa zao kwani
hawatakuwa na haja ya kubeba burungutu la pesa pindi watakapotembelea
Rock City Mall kwa kuwa kupitia huduma ya Airtel Money wataweza kuweka
au kutoa pesa pamoja na kufanya malipo mbalimbali wakati wote.
Wafanyabiashara pia wanaweza kuweka pesa za mauzo yao ya kila siku kwa njia rahisi na salama kupitia duka letu hili jipya”
Lyamba
aliongeza kwa kusema, duka hilo jipya litatoa huduma mbalimbali
zikiwemo kuunganishwa na huduma ya intaneti, huduma ya Airtel Money,
kurudisha namba iliyopotea, kufanya malipo ya ankra, kusajiri namba za
simu, muda wa maongezi, kujipatia modemu zenye ofa kabambe, pamoja na
simu za kisasa kabisa ikiwemo simu za Bravo Z10 inayokuja na ofa
maalumu ya kifurushi cha intaneti kwa shilingi 75,000
Tunaamini
duka hili litawawezesha wateja wetu kupata huduma zetu kwa urahisi sana
wakati wowote wanapotembelea Mall. Aliongeza Lyamba
Akiongea
wakati wa uzinduzi , Kamanda wa polisi Wilaya ya Ilemela, Switbert
Kisha alisema “ napeda kuchukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa
kuongeza maduka yake na kuhakikisha wanawafika wateja wake kwa urahisi
ili kutoa huduma bora za mawasiliano katika mkoa wa Mwanza. Duka hili
ndani ya Mall hii litawahakikishia watanzania usalama zaidi katika
kutumia huduma ya Airtel Money hivyo nawapongeza sana Airtel kwa
kuwahakikishia watanzanai usalama kupitia duka hili.
Huduma
za mawasiliano ni chachu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi ya jamii
na nchi kwa ujumla. Serikali inapongeza sana jitihada za Airtel
nakuwaomba waendelee kutanua huduma za zaidi na kuwafikiwa watanzania
wanaokaa maeneo ya pembezoni mwa nchi aliongeza Kisha
Duka
la Airtel ndani ya Rock City Mall Mwanza litakuwa likifunguliwa kuanzia
saa 8 asubuhi mpaka saa 11 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa na siku
ya Jumamosi duka litafunguliwa kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 7 mchana
Kamanda
wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha akikata utembe kuzindua
duka jipya la Airtel Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall
jijini Mwanza, akishuhudia Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja
Airtel, Adriana Lyamba.
Kamanda
wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha na Mkurugenzi wa kitengo
cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba wakikata keki kwa pamoja
wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity
shopping Mall jijini Mwanza, akishuhudia (kuli) ni wakala Mkuu wa Airtel
Money Mwanza, Mohamed Gichani.
Mkurugenzi
wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba akitoa maelezo
kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha kuhusu
huduma ya Airtel Money inayotelewa katika duka jipya la Airtel wakati
uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping
Mall jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha akiwa katika picha ya
pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana
Lyamba pamoja na wafanyakazi wa duka jipya la Airtel lililozinduliwa
ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza.