Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho
Jumatano kwa mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United
katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa
Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa
Sugar kutoka Manungu Turiani.
Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitano
kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji
Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani
jijini humo.
Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea
kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha
Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Jumapili African Sports watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la
magereza Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani jijii Tanga, huku
siku ya Jumatatu Mgambo Shooting wakicheza dhidi ya Toto Africans jijini
Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.