MKUTANO MKUU WA LAPF KUFANYIKA MACHI 10-11, 2016 UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA

March 02, 2016
 Viongozi meza kuu.

 Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF  James Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika machi 10 na 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti.
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja  na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.

Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.

Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.

" LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia" alisema Mlowe.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika  kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.

Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .

Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »