Mmoja wa vijana ambaye
anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya
wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa
na serikali akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU
kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda
kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati
walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu
Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na
Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya askari wakijiandaa
kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na
Mipango Posta jijini Dar es salaam.
Wanafunzi hao wakifurumushwa na
polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila kibali kwenda kumuona
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Wanafunzi hao wakitoka mbio baada ya kuamriwa na polisi kuondoka eneo hilo na kutawanyika.
Askari polisi wakizunguka maeneo mbalimbali kuangalia hali ya usalama.
Polisi wakiwazuia wanafunzi hao na kuwaamuru kutawanyika kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
Mmoja wa polisi akiwaamuru wanafunzi hao kutawanyika eneo hilo.
EmoticonEmoticon