Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi akizungumza
na vijana (hawapo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa
maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa
Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana
Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya
vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la
Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji Bw. Patrick Kipangula
(aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa
kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana
Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa maendeleo ya vijana
akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za
uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi kutoka Mamlaka
mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa, Taasisi za
kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za sekondari na Shule za msingi
wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha
kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa
jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi (watatu
kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na vijana wenye ulemavu wakati
wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la
Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia (waliokaa) ni
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi, wapili kushoto ni
Mwenyekiti wa kikao Bw. Godwin Kunambi, na wanne kulia (waliosimama) ni
Mkurugenzi msaidizi Vijana Bibi. Ester Riwa
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na; Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imedhamiria kuhakikisha
kuwa vijana wanakuwa na chombo chao chenye kujali utaifa, uzalendo na
maslai bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, rangi, hali za kiuchumi,
jinsia na maumbile kwa kuandaa kanuni zitakazolifanya Baraza la Vijana
Taifa kuwa huru na lenye haki.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Bw. Eric
Shitindi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleeo ya vijana
katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana
Taifa jana jijini Dar es Salaam.
“Nimuhimu kuunda Baraza kisheria
litakalokuwa na uwakilishi wa vijana wa makundi yote ili liweze kutumika
katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa” alisema Bw. Shitindi
Aidha Bw. Shitindi amelipongeza
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutunga sheria Na.
12 ya mwaka 2015 ya Baraza la Vijana Taifa ambalo litaleta maendeleo ya
vijana na nchi kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hicho
mwenyekiti aliyeteuliwa kuongoza mjadala huo Bw. Godwin Kunambi amesema
kuwa Vijana takribani 120 wamepata fursa adhimu ya kushiriki katika
uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa hivyo
kuwataka vijana hao kujadili mambo ya msingi yatakayowawezesha wananchi
wa Tanzania hususani vijana kutatua kero zao kupitia Baraza hilo.
Naye mwakilishi kutoka kundi la
watu wenye ulemavu Bw. Gaston Hemed Mcheka ameipongeza Serikali kutoa
nafasi kwa kundi la watu wenye ulemavu kuwa na uwakilishi kuanzia ngazi
ya kata hadi mkoa pindi Baraza la Vijana Taifa litakapoanza ambapo kundi
hilo litatumia nafasi hiyo kutatua changamoto zinazowakabili.
Kikao cha wadau wa maendeleo ya
vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la
Vijana Taifa kimeshirikisha takribani vijana 120 kutoka Mamlaka
mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa
vilivyosajiliwa, Taasisi za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za
Sekondari pamoja na Shule za msingi.
EmoticonEmoticon