Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za
rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo Fred Mosha
kilichotokea jana alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini
Dar es salaam.
Katika salamu hizo, TFF imewapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa
na marafiki kufuatia kifo hicho, na kusema wapo pamoja nao katika
kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Fred Mosha mpaka umauti unamfika, alikuwa mkuu wa kitengo cha habari
cha Tv/Redio Tumaini iliyopo jiini Dar es salaam na msiba upo nyumbani
kwa marehemu eneo la Mbagala Saku kwa Mkongo.
Mazishi yanatarajiwa kufayika kesho Jumatatu saa 9 mchana katika makaburi ya Kinondoni.
EmoticonEmoticon