KOMREDI KINANA AANZA KUCHAPA KAZI MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA KUZALIWA CCM SINGIDA

February 04, 2016
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la mtama la mkulima wa kujitegemea Elisha Mdaa (kushoto) katika Kata ya Mtamaa, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhimiza kila mwananchi kuchapa kazi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi Jengo la Ofisi ya CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho kutwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Unyianga, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho kutwa.

 Komredi Kinana akihutubia baada ya kushiriki ujenzi wa majengo ya shule ya Unyianga ambapo alihimiza wananchi kuwa na moyo wa kujitolea katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga tabia ya kuchapa kazi.
 Mkulima wa mfano wa shamba la mtama lililotembelewa na Komredi Kinana, Elisha Mbaa akielezea jinsi anavyotumia jembe la kukokotwa na ng'ombe  katika kilimo hicho, ambapo katika heka moja na nusu huvuna magunia 15 ya mtama na fedha zinazopatikana kwa kuuza mtama huo zinasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji mengine.
 Katibu wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Singida, akisoma risala ya pamoja ya wajasiriamali wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana mjini Singida leo. Komredi Kinana alitumia wasaa huo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi  kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Mwajuma wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi  kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Hawa Mtipa wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
 Komredi Kinana akizungumza na wajasiriamali mjini Singida leo
Ofisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa Wajasiriamali wa manispaa hiyo,  kuhusu uendeshaji wa mafunzo kwa waendesha Bodaboda pamoja na utekelezaji wa sheria mbalimbali za kodi ambazo mara nyingine si rafiki kwa wajasiriamali. Mkutano huo ulifanyika katika Jengo la Ofisi ya CCM ya Mkoa huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »