WATANZANIA wameshauriwa kujiunga na Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii iliyopo hapa nchini iili kuweza kupunguza ukali wa maisha
kwani itawasaidia kuepukana na gharama za matibabu ambazo zitakuwa zikilipwa na
mifuko husika wakati wanapokumbana na majanga mbalimbali.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Afisa Mwandamizi Rasilimali Watu
na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi na Uzibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
nchini (SSRA),Amina Ally wakati wa semina ya kuhamasisha maafisa wa mageraza
mkoani Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Alisema kuwa mifuko hiyo ina manufaa makubwa pamoja
na kupunguza ukali wa maisha kwa watumishi wa kada mbalimbali na kulinda
maslahi yao yakiwemo mahitaji ya kijamii ili kuweza kuondokana na gharama za
matibabu wanapokuwa wakiugua na majanga mengine.
Aidha licha ya hivyo mifuko hiyo imekuwa na faida
kubwa kwenye nchi katika uwekezaji inawafanya wanachama wa mifuko husika kupata
unafuu katika upatikanaji wa masuala yote ya msingi wakati panapokuwa
pamejitokeza mambo ya dharura na kwamba hukabiliana nayo bila kujali hali ya
kipato au michango ya muhusika.
“Ukiangali
mifuko hii ya hifadhi ya Jamii imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa jamii lakini
pia inasaidia kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha uliopo sambamba na
kupunguza umaskini kwa watanzania waliojiunga nayo kwenye kunufaika na mambo
mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu “Alisema Amina.
Hata hivyo alitaja mifuko ambayo alidaia kuwa ndio
kimbilio kubwa la watanzania walio wengi hapa nchini kuwa ni Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF),Mfuko
wa Pensheni wa (PPF),Mfuko wa Pensheni wa Wafanyakazi wa Serikali (GEPF),Mfuko
wa Pensheni wa (LAPF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).
Alisema kuwa licha ya kupatikana mafanikio kwenye
mifuko lakini zipo changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo wafanyakazi wa sekta
zisizokuwa rasmi kushindwa kujiunga kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii hivyo
aliwashauri washiriki wa semina hiyo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri
kuielimisha jamii namna wanavyoweza kujiunga nayo ili waweze kunufaika.
EmoticonEmoticon