MSWADA WA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

December 21, 2015
Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano maalumu na wazee wa Jiji la Tanga leo
Serikali inatarajia kuwasilisha  mswada wa sheria katika bunge la Mwezi wa tisa  kwa ajili ya kuundwa kwa sheria ya wazee ili kuhakikisha sera ya wazee inafanyakazi ipasavyo hapa nchini .
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Alhaj Abdulla Lutavi akitoa neno kwenye mkutano huo

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri  wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea katika mkutano maaluma na wazee wa Jiji la Tanga leo


 Alisema kuwa Mswada huo utakapofikishwa bungeni na wabunge kuuridhia itasaidia kusimamia ufanyaji kazi wa sera ya wazee ambayo ilikuwa imetungwa siku nyingi lakini ilikuwa haifanyiwakazi kwa kukosa muongozo.

“Licha ya serikali kujitahidi kupunguza changamoto za wazee lakinia tunajua kuwa bado  matatizo mengi ya wazee ambayo yanahitaji ufumbuzi na usimamizi wa kisheria hivyo kwa jitihada hizo zitawezesha kumaliza changamoto hizo”alisema Waziri Mwalimu.

Moja kati ya wazee wa mkoa wa Tanga,Alhaji Kassim Kisauji akiuliza swali kwenye mkutano huo
Aidha aliziagiza Halimashauri zote nchini kuhakikisha zinawatambua wazee walioko katika maeneo yao hususani wale waliofikia umri wa miaka 60 na kuendelea.

“Niwaombe katika utambuzi huo muhakikishe unawaainisha wazee wanaojiweza na wale wanaojiweza ilikuhakikisha mnawatengeneza utaratibu maaluma wa kupata mahitaji yao muhimu kama ilivyoainishwa kwenye sera”alisisitiza

Baadhi ya wazee wa mkoa wa Tanga wakifuatilia matokeo mbalimbali kwenye mkutano huo na Waziri Ummy
Hata hivyo Waziri Mwalimu alisema kuwa moja ya mikakati ya wizara yake ni kuhakikisha wamewasajili wazee wapatao laki mbili na kuwaingiza kwenye mpango wa matibabu bure .

Alisema kuwa licha ya idadai hiyo kuwa ni ndogo lakini anaamini mpango huo ukipata usiamamizi mzuri unaweza kuwasaidia wazee kupata huduma bora za matibabu katika ngazi zote za wilaya hadi rufaa.

 
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa asasi ya wazee mkoa wa Tanga TARINGO Fredorin Mbunda aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kuongeza kiwango cha fedha za pesheni kwa wazee ili iendane na hali halisi ya mazingira ya sasa.
 

Alisema kuwa peshen iliyopo inawasaidia kupata milo miwili tu kwa siku hali ambayo inasababisha wazee wengi kuishi katika maisha ya tabu na duni kwa kiasi kikubwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »