MAKAMPUNI YA MAWASILINANO YA SIMU YATAKIWA KUBORESHA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAO ILI KUONDOA MALALAMIKO

December 17, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Desemba 15 -2015 ).Picha Emanuel Madafa  

Mwenyekiti Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za  Mawasiliano (TCRA-CCC)Ndugu Stanley Mwabulambo (kulia) pamoja na Meneja wa Mawasiliano TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini Mhandisi Lilian Mwangoka wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika ufunguzi wa semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro katika semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya wakifatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Abbasi Kandoro.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza katika semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha  watumiaji wa wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo akitoa neo katika semina hiyo ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa Huduma za mawasiliano  Mkoa Mbeya Desemba 15-2015 katika ukumbi wa Mkapa jijini mbeya.

Wadau wakifuatilia mkutano 

Kaimu Katibu mtendaji Baraza la Ushauri watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA-CCC Ndugu  Mary Msuya akiwasilisha maada kwa wanasemina juu ya haki na wajibu wa Mtumiaji wa huduma za Mawasilino  katika semina hiyo yenye lengo la kuelimisha na kuhamsisha watumiaji wa huduma hizo Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya.


Mhandisi toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina hiyo.

Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina .

Mjumbe wa Baraza la Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Ndgugu Nyanda Shuli akitoa Maada juu ya Muundo ,Kazi na Majukumu ya Baraza la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano katika semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.

Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo.


Picha ya pamoja na Meza Kuu.

Na EmanuelMadafa,Mbeya(jamiimojablogu )
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya  huduma za Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha yanaboresha huduma zao  kwa kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino hayo.
Amesema moja ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino hayo ni pamoja na kuweka matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa kiasi cha pesa pasipo makubalino.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa huduma hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo yakahakikisha yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na thamani inayolipwa na watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza majukumu yao kwa watumiaji kama yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni za leseni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo za mawasiliano ya simu kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu badala ya kujingiza katika matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa maadili katika jamii pamoja na uchochezi.
 Amesema kuwa sheria ya makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa  dhidi ya mtu au kikundi kitakacho husika na upotoshwaji wa aina yoyote .
Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na adhabu zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari na mawasilino.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA- TCCC  kuendelea  kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na kuelewa  kero na matalajio ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni yote yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za utangazaji na huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao ya huduma zao nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za mawasiliano.
Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza pia limeunda kamati ya watumiaji  wa huduma za mawasililiano kwa mkoa wa mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo walichaguliwa kutoka miongoni mwa wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni kuelimishajamii juu ya haki wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko sanjali na kupokea toka kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.

Mwisho.
KAWAIDA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »