MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na
kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili,
sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa
na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na
kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11,
2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa
Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo
walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika
suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake
ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na
kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie
Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
Dec 11, 2015 kwa mazungumzo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe,
wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10,
2015 kwa mazungumzo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan,
akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad,
baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa
Ndilowe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es
Salaam,jana Dec 10, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia
Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini
Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Idara
ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa
Balozi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam leo Desemba 11, 2015.
Picha na OMR
EmoticonEmoticon