BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA 'TUMA PESA NA SIMBANKING SHINDA PASSO'

December 11, 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi  wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja mku, Tulli mwambapa akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Wageni.
Zawadi za washindi.
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi akikabidhiwa zawadi ya Solar Panel
Martin Mmari akimkabidhi Deo Ndejembi funguo ya gari aina ya Passo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari (katikati), akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Maria Minde, wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akimkabidhi funguo ya gari mshindi wa shindano la ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Hellen Solomon.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari.
Deo Ndejembi akiwa ndani ya gari aina ya Passo.

Dar es Salaam, Tanzania
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Bunge, Sera, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ni miongoni mwa washindi watatu wa magari aina ya Toyota Passo yaliyotolewa na Benki ya CRDB.


Kuanzia Februari, 2015 benki hiyo ilianzisha shindano la Tuma pesa na simubanking, shinda Passo ili kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kwa simu za kiganjani ambapo kila mwezi kwa mwaka mmoja, mteja mmoja wa benki hiyo alishinda gari.

Jana Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei aliwaongoza watendaji wengine wa benki hiyo kugawa zawadi kwa washindi watatu wa Septemba, Oktoba na Novemba.
Pamoja na Mavunde aliyeshinda gari hilo Septemba, washindi wengine na miezi yao kwenye mabano ni Maria Minde (Oktoba) na Hellen Achimponta (Novemba).
Akizungumzia mafanikio ya Tuma pesa na simu banking, shinda Passo, Dk. Kimei alisema wateja wa huduma hiyo wameongezeka kutoka 830,000 mwaka 2013 hadi 1,200,000 mwaka 2015 ambapo jumla ya miamala 10,152,605 imefanyika na kuiingizia benki Sh. milioni 695.
“Matumizi ya huduma za simbanking yanamuweka mteja karibu zaidi na benki… anaweza kufanya huduma yoyote akiwa popote wakati wowote bila kufika benki.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »