WATEJA WA TIGO JIJINI TANGA KUNUFAIKA KWA KUPATA MTANDAO WA INTANETI WENYE KAZI KUBWA ZAIDI BAADA YA UPANUZI WA HUDUMA YA 4GLTE

November 26, 2015





WATEJA wa Tigo waishio jijini Tanga wanatarajia kunufaika kwa kupata mtandano wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4GLTE hadi kufikia kwenye jiji hili lililopo kaskazini mwa Tanzania.
Teknologia ya 4GLTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kanda ya Pwani, Goodluck Charles wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa Upatikanaji wa Teknologia ya 4GLTE jijini Tanga, uliofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Jijini hapa.

Alisema kuwa upanuzi huo umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji wa huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu ambayo ni kielelezo cha jinsi ambayo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya kidigital katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika mstari wa mbele wa kutumia teknologia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania.

Aidha alisema kuwa mtandao wa 4G LTE una kazi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandano wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype kwani huduma hiyo inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora wa hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.

  “Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waisio Tanga kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na intaneti yenye kasi zaidi,Tanga ni makao makuu ya taasisi nyingi za kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kitovu cha Utalii nchini “Alisema Goodluck.
 

…..Tunapenda kuwatangazia wateja wetu wa Tigo kwamba bei ya vifurushi vyetu vya 4GLTE ni sawa na bei ya vifurushi vya intaneti vya 3G kwa hivyo mteja haitaji kulipia zaidi kwa ajili ya kutumia huduma ya 4GLTE na wateja wote wa Tigo 4GLTE watanufaika na promosheni ,kila watakapoongeza salio la shilingi elfu moja,atapata MB 500 za bure kama bonasi.
Alisema kuwa uzinduzi wa upatikanaji wa huduma ya 4GLTE kwa ufanisi jijini Dar es Salaam na Arusha na miji mingine katika mikoa sita ambapo huduma hiyo itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa  ni Dodoma,Morogoro,Moshi na Mwanza.


Mkurugenzi huyo alisema kuwa jambo hilo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G LTE nchini Tanzania ambapo lengo lao kuu ni kufanikisha huduma hiyo katika kila kona ya nchi ifikapo mwaka ujao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »