Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea
mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa
baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na
Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa
ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo
Daktari Bingwa wa Magonjwa
Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa
wagonjwa.
Meneja Mauzo barani Afrika,
Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo
imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………………..
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator ya kumsaidia mgonjwa
kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000 sawa na Shilingi
milioni 80.
Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland .
Akikabidhi mashine hiyo mpya na
kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka
Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea
kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya
matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya
miaka miwili.
Akipokea msaada huo Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo
ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali
hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo
bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi.
Akielezea kuhusu mashine hiyo
Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema
mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa
maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo
inaonyesha .
EmoticonEmoticon