Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, Charles Boniface Mkwasa ameendelea na mazoezi ya kukinoa kikosi
chake kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es
salaam kuwania kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Baada ya kufanya mazoezi kutwa
mara mbili (asubuhi na jioni) kwa siku tatu, leo Ijumaa kocha Mkwasa
amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi mara moja wakati wa jioni
katika uwanja wa Edenvale.
Mkwasa amesema baada ya kufanya
mazoezi ya kujenga mwili, stamina, na pumzi sasa kazi anayoifanya ni
kutengeneza mfumo wa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo dhidi ya
Mbweha wa Jangwani.
“Tulipofika tulianza na mazoezi
ya utimamu wa mwili, stamina na pumzi ili kuhakikisha wachezaji wote
waliopo kambini wanakuwa katika kiwango kimoja kutokana na kuwa
wachezaji wanatoka katika timu tofauti na zenye walimu na mifumo
tofauti” Alisema Mkwasa.
“Sasa baada ya wachezaji kufanya
mazoezi kwa siku nne kuweka uwiano sawa kiwango cha kimazoezi (fitness
level) kwa sasa tunafanya kazi kutengeneza mfumo na jinsi ya uchezaji”
aliongeza Mkwasa.
Stars inaendelea na mazoezi leo jioni na kesho Jumamosi itafanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Edenvale
NB: Namba ya Afisa Habari wa TFF aliyepo nchini Afrika Kusini +27 78 641 1595
EmoticonEmoticon