Dkt.Maria Mashingo akila kiapo
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete
baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015.
Prof.Elisante Gabriel akila kiapo
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete baada ya
kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo, Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015,awali Prof.Gabriel
alikuwa Naibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
Dkt.Jakaya Kikwete akimpongeza Bw.Eliakim Maswi mara baada ya kumaliza
kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam,Bw.Maswi ameteuliwa kuwa Katibu
Tawala Mkoa wa Manyara.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Gabriel
(katikati)akipongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi
Sihaba Nkinga (kulia) ambaye amehamishiwa Wizara ya Wanawake,Jinsia na
Watoto pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Assah Mwambene
(Kushoto),mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(Kulia) akiwa katika picha na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika Bw.Zidikheri Mundeme mara
baada ya kuapishwa ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(kulia) akiwa katika picha na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Hab Mkwizu mara baada
ya kuapishwa ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete (watano kulia) pamoja na Katibu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue (watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na
Makatibu Wakuu waliyoteuliwa mara baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar
es Salaam Oktoba 24,2015.
Picha zote na Anitha Jonas – MAELEZO.
EmoticonEmoticon