Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua mradi wa kusaga kokoto
uliopo katika kijiji cha Pongwe Msungura Wilayani Bagamoyo leo. Kulia ni
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi, Wapili
kulia, ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael
Muhuga,wapili kushoto ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe.Yasemin Eralp,
watatu kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ANIT ASFALT Bwana
Semih Yaran, na wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika kijiji
cha Pongwe Msungura kuzindua mradi wa kusaga kokoto.Aliyesimama pembeni
ya Rais ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga.
Mradi huu unaendeshwa kwa ubia kati ya SUMA JKT na kampuni ya ANIT
ASFALT ya Uturuki kwa mtaji wa shilingi Bilioni Tano na milioni mia moja
ambapo SUMAJKT inamiliki asilimia 30 sawa na shilingi Bilioni moja na
milioni mia sita na themanini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Pongwe Msungura wakati wa ufunguzi
wa mradi wa kusaga kokoto.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael
Muhuga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaga kokoto.kulia ni Mkuu wa
mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe.Yasemin Eralp akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi wa kusaga kokoto leo.
Kikundi cha sanaa cha JKT kikitumbuiza wageni wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa kusaga kokoto.
(picha na Freddy Maro)
EmoticonEmoticon