Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama
Salma Kikwete akimnadi mgombea Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa
Mpilipili huko Lindi Mjini tarehe 12.10.2015.
Mgombea
Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete mara baada ya kumwombea
kura kwa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili tarehe 12.10.2015. Aliyesimama
kulia ni Mgombea Ubunge katika Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Mama Salma Kikwete akiwa katika kijiji cha
Ngunichile kilichoko katika Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya kuwanadi
wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
tarehe nchini tarehe 25.10.2015. Katika mikutano hiyo Mama Salma
alimnadi Dkt. John Magufuli kwenye urais na Ndugu Hassan Elias Masala
kwenye Ubunge wa Jimbo la Nachingwea na Madiwani wote katika wilaya hiyo
tarehe 13.10.2015.
Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
Wananchi
wa mkoa wa Lindi wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea
mabadiliko ya kweli katika maisha yao kwani kuna baadhi ya watu
hawapendi kufanya kazi huku wakisubiri mabadiliko.
Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Ngunichile na Mbaya vilivyopo katika majimbo ya Nachingwea na Liwale waliohudhuria
mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na
urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema mabadiliko
ya kweli hayawezi kupatikana bila ya kufanya kazi kwani kuna baadhi ya
watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni
kucheza pool huku wakisubiri mabadiliko.
“Hata
katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi
ni msingi wa maendeleo, hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi
kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako”.
“Ndugu
zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya
tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta
uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya
vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu
hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna
maendeleo”, alisisitiza.
Mama
Kikwete alisema yeye kama MNEC anadhamana kubwa ya kuhakikisha
anakisemea na kukipigania chama chake na kuwataka wananchi hao
kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa kufanya hivyo wataitunza Amani ya
nchi na kuzidi kudumisha upendo katika jamii yao.
Aidha
aliwasihi wananchi hao kutokubali kurubuniwa na kitu chochote bali
wazitunze kadi zao za kupigia kura na siku ya uchaguzi ikifika
wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi na
kuwachagua viongozi kutoka CCM ambao watawaletea maendeleo ya kweli.
Kwa
upande wake mgombea ubunge jimbo la Nachingwea Hassan Massala aliahidi
kama atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo atasimamia ilani ya uchaguzi ya
CCM na kuhakikisha huduma za elimu zinaboreshwa hii ni pamoja na shule
kuwa na vitabu na walimu wa kutosha na kujenga nyumba za walimu ili
watoto wapate elimu bora. Ataboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na dawa zinapatikana kwa
wakati.
Massala
alisema, “Katika jimbo hili, maeneo ya mjini kuna maji ya kutosha
lakini kijiji cha Ngunichile kuna tatizo ingawa vyanzo vya maji vipo.
Nitahakikisha maji yanapatikana. Kuhusu umeme Serikali inampango wa
kusambaza katika vijiji vyote, nguzo zimeanza kusambazwa
kinachohitajika ni kusimamia ili zoezi hili liende haraka”.
Mgombea
huyo wa nafasi ya Ubunge alimuomba Mama Kikwete awasaidie ili mnara wa
mawasiliano ya simu uweze kujengwa katika kata ya Ngunichile kwani
eneo hilo linashida ya mawasiliano.
“Ukiwa
katika kijiji hiki huwezi kuwasiliana na mtu yeyote kwa njia ya simu
kwa kuwa hakuna mnara wa mawasiliano. Hivi sasa simu ni pesa na simu ni
Benki tunaomba Mama yetu utusaidie ili mnara wa mawasiliano ujengwe
katika kijiji hiki”, Massala aliomba.
Kuhusu
ombi la kujengewa mnara wa mawasiliano ya simu katika kijiji hicho
ambacho ni kata ya Ngunichile Mama Kikwete aliahidi kulifanyia kazi na
kulifikisha kunakohusika.
Naye mgombea
ubunge wa jimbo la Liwale Faith Mitambo aliwaomba wananchi wamchague
ili aendelee kuwatumikia kwa kipindi kingine cha miaka mitano na
kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana katika jimbo hilo.
Mitambo
alisema, “Ilani ya uchaguzi ya CCM inasema itaendelea kuboresha huduma
ya afya na ndani ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi Zahanati ya kijiji cha
Mbaya itakuwa kituo cha Afya. Aidha Serikali imetenga zaidi ya shilingi
bilioni tatu kwa ajili ya kuhakikisha umeme unapatikana vijijini kati
ya vijiji hivyo kimojawapo ni kijiji hiki.
“Nawaomba
kura zenu ili mtuchague viongozi kutoka CCM ambao ni madiwani, mbunge
na rais ili tuweze kusimamia na kutekeleza kwa vitendo na kuhakikisha
yale yote yaliyoandikwa katika ilani ya uchaguzi yanatekelezwa”,.