William Rutto – Hongera Rais Kikwete kwa kukuza tasnia ya filamu Nchini Tanzania

August 05, 2015
Makamu wa Rais Wa Kenya, Mh William Rutto akifungua maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yajulikanayo kama JAMAFEST kwa kuwakaribisha washiriki kutoka nchi zote za Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Kenyatta uliopo jijini Nairobi, Nchini Kenya. Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta kabla ya ufunguzi wa maonyesho ya JAMAFEST 2015
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Makumira wakitoa burudani ya ngoma wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamadanu Festival yajulikanayo kama JAMAFEST katika ukumbi wa mikutano wa kimtaifa wa Kenyatta.
 Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya JAMAFEST 2015 kutoka nchini Burundi wakiwa katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto amempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na kupelekea Wananchi wa Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki kupenda zaidi filamu za Kitanzania ambazo zimekuwa na soko kubwa sana katika nchi za Jumuiya ya Mashariki.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni lijulikanalo kama JAMAFEST 2015 linalofanyika katika viwanja vya ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta uliopo katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya, Mh Rutto pia aliwapongeza marais wa nchi za Jumuiya Ya Afrika Mashariki kwa juhudi zao katika Shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi, utamadanu na Michezo.
Mh Rutto alitoa pongezi kwa Rais Wa Rwanda, Mh Paul Kagame kwa kutoa mchango mkubwa sana katika Michezo kwa kudhamini Michuano ya Kombe la Kagame ambapo mwaka Huu Timu ya Azam FC kutoka Nchini Tanzania iliweza kuibuka mshindi kwa kuifunga Timu yao ya Kenya Gor Mahia kwa mabao Mawili kwa sifuri. Vilevile Mh Rutto aliipongeza timu ya Azam kwa kuweza kuwa mabingwa wa Kombe la Kagame kwa kuweza kuifunga timu yao ya Kenya ya Gor Mahia na kuweza kuibuka washindi wa Kombe la Kagame linalodhaminiwa na rais wa Rwanda Nh Paul Kagame. Mbali na Kumpongeza rais wa Rwanda na Tanzania pia Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto aliwapongeza pia rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kuwa mstari wa mbele katika Kukuza utamaduni wa Nchi yake huku Rais wa Burundi akipongezwa Kwa Kuweza kusakata kabumbu na kusema kuwa anatamani awe rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).
Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni (JAMAFEST) yameshirikisha nchini zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Kila Nchi mwanachama wameweza kuonyesha Bidhaa zao pamoja na utamaduni wao. Maonyesho haya ya JAMFEST hufanyika kila baada ya Miaka Miwili ambapo mwaka 2013 Maonyesho haya yalifanyika nchini Rwanda na mwaka huu yanaendelea kufanyika Nchini Kenya huku mwaka 2017 maonyesho haya yanatarijiwa Kufanyika Nchini Tanzania.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »