TANGAZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
inawakaribisha wananchi na wadau wote katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Tarehe 16-23 Juni, 2015
Mahali: Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
Kaulimbiu: “Utumishi wa Umma
katika Bara la Afrika ni Chachu ya Kuwawezesha Wanawake, Kuongeza
Ubunifu na Kuboresha Utoaji Huduma kwa Umma”.
Ushauri na Huduma mbalimbali zitatolewa na wataalamu kutoka katika Taasisi za umma bila malipo.
Ufunguzi utafanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb), na siku ya kilele Tuzo
zitatolewa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi.
Tarehe 17 Juni, 2015 Kongamano la
Wiki ya Utumishi wa Umma litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na ufunguzi utaongozwa na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue, na Msemaji Mkuu atakua Katibu Mkuu
Kiongozi mstaafu Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Hakuna kiingilio katika maadhimisho haya, wananchi wote mnakaribishwa.
………………………..
Limetolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
K.n.y; KAIMU KATIBU MKUU (UTUMISHI)
EmoticonEmoticon