Wachezaji
wa timu ya taifa Taifa Stars wakiwa katikati ya msitu wa wachezaji wa
timu ya Madagascar katika mchezo wao wa jana ambapo ilifungwa magoli
2-0.
Timu zikiingia uwanjani.
…………………………………………………………………………..
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe
la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 – 0 na Madagascar, mchezo
uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo
huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya
makundi,kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba
dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.
Katika mchezo huo wa jana, Taifa
Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na
kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa
Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya
ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za
washambuliaji wa Madagascar.
Mara baada ya mchezo huo, kocha wa
Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba
hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.
“Timu yangu haikucheza vizuri,
haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu
wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo
huo” alisema Nooij.
Mpaka sasa kundi B la linaongozwa
na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa
na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho
utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo
fainali.
Kufuatia Taifa Stars kupoteza
michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano
hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga
michuano hiyo pia.
Stars inatarajiwa kurejea nyumbani
Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya
Lesotho utakochezwa kesho jioni.
EmoticonEmoticon