Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu
nchini jana imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya
inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing)
Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo
ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la
hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.
Huduma
hii ya Airtel Zone imezinduliwa kwa mara ya kwanza na Airtel ili
kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano ya simu za
mkononi na kutoa fursa kwa wateja wake kuongea zaidi kwa gharama nafuu
mara tu watakapo jiunga kwa kupiga namba 107 na kufuata maelekezo au
kupiga *149*39# kisha kuchagua) ‘
Akiongea wakati wa
uzinduzi Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema”
uzinduzi wa punguzo la gharama za kupiga simu ni uthibitisho wa dhamira
ya kampuni ya Airtel kuwapatia watanzania dili lenye thamani halisia ya
fedha zao na kuwawezesha watu wengi zaidi nchini kuwasiliana kirahisi.
Lengo letu ni kuendelea kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu
ili kukithi mahitaji ya watanzania wote. Wateja wetu watakaojiunga na
huduma ya “Airtel Zone” kuanzia leo, sasa hivi wataweza kupiga simu na
kupata punguzo la hadi asilimia 99 na punguzo hili litategemea mahali
alipo mteja”
“Hii ni punguzo
litakalosaidia sana wateja wa Airtel kupata unafuu wa kuwasiliana
kibiashara, masomo au kwa kuwasiliana na ndugu jamaa au wapendwa wao
bila kuwa na wasiwasi juu ya gharama zao za simu” alieleza bw, Nyakundi
Tunaamini huduma hii ya
“Airtel Zone” imekuja kwa wakati muafaka wakati mawasiliano ya simu za
mkononi ni nyenzo muhimu katika ukuzaji wa shughuli za kiuchumi na za
kijamii aliongeza Nyakundi
Akifafanua zaidi kuhusu
huduma hii Mkurugenzi wa Mawasilaiano Bi Beatrice Singano Mallya,
alisema” punguzo la gharama litategemea mahali mteja alipo na muda
anaopiga simu, mteja atapata ujumbe utakaomuonyesha kiwango cha punguzo
anachopata kwa mahali alipo, alikadhalika mteja anaweza kupiga
*149*39*0# ili kuangalia kiwango cha gharama ya kupiga simu. Huduma hii
ya “Airtel Zone” ni kwa wateja wa malipo ya awali na punguzo hili
litatumika kupiga simu za ndani tu .
Sambamba
na hilo mteja atakayekuwa na kifurushi cha muda wa maongezi kama vile
Airtel yatosha na vifurushi vingine punguzo litaanza pale tu kifurushi
chake cha muda wa maongezi kitakapoisha.
Kuujiunga ni rahisi, bure na mara moja tu, piga 107 ufate maelekezo au piga *149*39#” aliongeza, Singano Mallya.