Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu
Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani
wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la
Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5
yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari
katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu
Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah
Maongezi, Mkurugenzi wa Afya kutoka Taasisi ya WAMA.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu
Sophia Mjema akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya Shule
za Sekondari katika Wilaya ya Temeke walioshiriki katika mafunzo ya
kuzuia mimba za utotoni. Mafunzo hayo yalifanywa na Taasisi ya WAMA
ikishirikiana na Shirika la Engender Health kwa ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani, USAID. 
Baadhi ya wanafunzi na walimu
kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakiimba wimbo wa
kumkaribisha mgeni rasmi alipokuwa akiingia ukumbini.
Meneja wa Uragibishi na
Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wana wake na Maendeleo, Ndugu Philomena
Marijani akitoa maelezo ya awali kuhusiana semina ya siku 5 ya kuzuia
mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke
iliyofanyika huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
kuzuia mimba za utotoni kutoka Wilaya ya Temeke wakimsikiliza salamu
kutoka Taasisi ya WAMA zilizotolewa na Meneja wa Uragibishi na
Mawasiliano wa Taasisi ya hiyo Ndugu Philomena Marijani wakati wa
sherehe ya kufunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe
17.5.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu
Sophia Mjema akitoa hotuba ya kufunga rasmi mafunzo ya kuzuia mimba za
utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Wilaya ya Temeke yaliyofanyika
Kibasila Sekondari.
Washiriki wa semina ya siku 5 ya
kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika
Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati
akifunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Meneja wa Kanda ya Pwani kutoka
Shirika la Engender Health, Dkt. Martha Kisanga akimkabidhi Mkuu wa
Wilayaya Temeke Ndugu Sophia Mjema maelezo ya mradi wa kuzuia mimba za
utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Temeke unaosimamiwa kwa pamoja
baina ya Shirika lake na Taasisi ya WAMA wakati wa sherehe ya kufunga
mafuzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya kuzuia
mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke
wakifuatilia kwa makini sherehe za kufunga mafonzo yao huko Kibasila
Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu
Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa
mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika
Wilaya ya Temeke huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu
Sophia Mjema akiwaaga washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni
kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke huko Kibasila
Sekondari tarehe 17.4.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI
EmoticonEmoticon