
Polisi wakie;ekea emeo la tukio
Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu hizo wakipakiwa katika gari la FFU

***********
Na MatukiodaimaBLOG
VURUGU
kubwa zimetokea leo katika eneo la Ipogolo mjini Iringa na kupelekea
askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kutumia mabomu ya machozi
kuthibiti vurugu baada ya mtoto wa miaka kata 6 kugongwa na gari wakati
akifanya biashara ya kuuza mbogo mboga .
Wananchi
wanaosadikika kuwa na hasira kali walianza kuwashambulia askari polisi
waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe kwa madai ya kuchelewa kufika
eneo la tukio.
Wakizungumzia
tukio hilo kwa mwandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi walisema
kuwa mtoto huyo aligongwa majira ya saa 7 mchana na zaidi ya saa moja
baada ya kutoa taarifa polisi ndipo walipofika eneo la tukio jambo
lililowakwaza wananchi hao .
Walisema
kuwa mbali ya polisi hao kufika pia tayari baadhi ya askari waliopo
eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo kwa kushirikiana na wananchi
walifanikiwa kulikamata gari ambalo lilisababisha ajali hiyo .
Alisema
Neema Sanga kuwa wakati tukio la kugongwa mtoto huyo likitokea alikuwa
jirani na eneo hilo katika msiba na kuwa wakati akiwa ameingia ndani ya
nyumba hiyo yenye msiba kusaidia kugawa chakula ghafla alipata taarifa
kuwa wananchi wameanza vurugu kwa kuchoma moto matali katika barabara
hiyo kuu ya Iringa- Kilolo.
Hata
hivyo alisema kuwa tukio hilo lilichukua zaidi ya dakika 45 polisi hao
wa FFU kufika na kuanza kutuliza vurugu hizo kwa kupiga mabomu ya
machozi kuwatawanya wananchi zaidi ya 500 waliokuwa wamekusanyika eneo
hilo kuzuia magari kuendelea kupita katika barabara hiyo huku baadhi yao
wakitaka kufunga barabara kuu ya Mbeya - Iringa ambayo haihusiki ka
bisa na eneo lililotokea tukio hilo.
"
Ni kweli mtoto kagongwa na gari na kufa tukio ambalo ni kusikitisha
sana na polisi baada ya kupigiwa simu wamefika eneo la tukio na kuchukua
maiti ya mtoto huyo lakini tunajiuliza kwanini vijana hao kuanza
kuwapiga mawe polisi na kufanya vurugu wakati gari lililogonga mtoto
huyo likiwa limekamatwa .." alihoji Bi sanga
Kuwa
kwa upande wake hakuona sababu za polisi kupigwa wala wananchi hao
kuchoma moto barabara wakati ajali hiyo kama ajali nyingine na tayari
gari lililosababisha ajali likiwa limekamatwa .
Bi
Sanga alisema wakati mwingine polisi wanalalamikiwa kuwa wanatumia
nguvu zaidi ila kwa tukio hilo lawama zake anazipeleka kwa wananchi
wenzake ambao walionyesha kufanya vurugu kwa kuchomo moto barabara hiyo
ya lami na kupiga polisi huku wakitambua wazi polisi si waliosababisha
ajali hiyo.
Huku
kwa upande wake mmoja John Kalinga akiomba serikali kupitia wizara ya
miundo mbinu kuangalia uwezekano wa kuweka matuta katika eneo hilo kwa
madai kuwa hii ni ajali ya pili kutokea na kusababisha vifo toka eneo
hilo lilipowekwa lami .
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia baadhi ya vijana wakikimbilia kujificha
katika nyumba moja iliyopo eneo hilo ambayo ilikuwa na msiba huku baadhi
yao wakijifungia katika maduka na bar zilizopo eneo hilo kabla ya
polisi kuwafuata na kuwakamata huko walikojificha na kuwaacha wale
waliokimbilia msibani .
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza kupatikana
kuzungumzia tukio hilo huku idadi ya vijana waliokamatwa kwa tuhuma za
kuhusika katika vurugu hizo zaidi ya 20 walionekana wakipagiwa katika
magari ya polisi.
EmoticonEmoticon