Wasimamizi
wa redio za jamii wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa redio za Jamii, Joseph Sekiku akiongea machache kabla ya
kuwagawia wasimamizi wa redio za jamii wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, akiwagawia
wasimamizi wa redio za jamii katiba iliyopendekezwa iliwekwa kwa nji ya
sauti.
………………………………………………………………………
Wakurugenzi
na viongozi mbalimbali wa Radio za jamii wamethibitisha kupokea na
kuanza kurusha Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya sauti, makala na
michezo ya radio iliyoandaliwa na Kampuni ya Focus Media na COMNETA
zenye maudhui ya katiba inayopendekezwa.
Wakizungumza
na Focus Media ambao ndio waandaaji na wasambazaji wamekiri kwamba
wamepokea kwa wakati muafaka, kwani hawakuwa na chanzo sahihi cha kupata
maudhui yanayohusu elimu ya uraia na uchaguzi mkuu na kura ya maoni.
Baadhi
ya wasimamizi wa radio zilizo katika mtandao wa radio za kijamii
Community Media Network of Tanzania ambao wamethibitisha kupokea
vitendea kazi hivyo ni Bw. Ali Khamis Mtwana, Mkurugenzi Mtendaji wa
Tumbatu Island Community Radio, Bw. Anton Masai Triple A FM Arusha, Dr.
Lazaro Ole Mongoi Mkurugenzi Mtendaji wa IDEA Radio, Henry Bernard,
Adelina Lweramla, Jackson Mollel, wa ORS FM Arusha, Edwin Mpokasye,
Radio Fadhila Mkurugenzi Radio Kwizera- Ngara.
Vipindi
vinapokuwa vikiruka hewani wasikilizaji wamekuwa wakishiriki kwa kupiga
simu na kuuliza maswali ilikuelewa zaidi Katiba Inayopendekezwa.
Wengine
wanapiga simu kupongeza na mnamichezo ya radio ilivyoratibiwa vizuri na
ikielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali muhimu.
ILI KUSIKILIZA VIPINDI HIVI VYENYE MAUDHUI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA TEMBELEA
www.facebook.com/KatibaInayopendekezwaTanzania