Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda
,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu
ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini
mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajili na kutambulika
na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.
Katibu
wa Umoja wa Boda Boda Moshi mjini akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliofanyika ,Stendi Kuu kata ya
Mawenzi Moshi mjini.
Wafanyabiashara
wa soko la kati,Moshi mjini wakiwa wamefunga njia kuzuia msafara wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana usipite mpaka wawasilishe
kero yao ya kufungiwa soko kwa mwaka mzima na uongozi wa halmashauri ya
mji kwa maelezo ya kupisha ukarabati ambao haujafanyika.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye
mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma risala ya wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara
ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuingia kwenye soko la kati, Moshi mjini
mkoani Kilimanjaro ambalo lilifungwa kupisha ukarabati ambao mpaka sasa
ni mwaka 1 hakuna kilichofanyika na wafanyabiashara wanaishi maisha
magumu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa
soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
Ukuta wa soko la kati Moshi mjini ukiwa na matangazo yanayozuia kufanya biashara
Katibu
wa Vikoba kata ya Kongoroni Mariam Chawapoma akisoma risala ya kikundi
chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Wanachama wa Vikoba wakishangilia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba
kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye
wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada
ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.
Wajasiriamali na mama lishe wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kata yao ya Njoro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajasiriamali pamoja na mama lishe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Idd
Juma
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati
akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule
ya msingi Mandela.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu
Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia
kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM
kuongoza mji wa Moshi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini
mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na
kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali
maendeleo yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini
kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela
na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa
kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia picha ya gari
alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabala halijafanyiwa
ukarabati na Chuo cha Ufundi Veta, Moshi mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari
alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za
kutafuta uhuru,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye gari
alilotumia Baba wa Taifa wakati wa harakati za kutafuta uhuru.
Wananchi
wakiuaga msfara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara
baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Mandela,Bomambuzi, Moshi Mjini.


























EmoticonEmoticon