JESHI la
Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye alihusika
katika tukio la uporaji wa silaha askari eneo la barabara ya nne na tano mtaa
wa makoko jijini Tanga Januari 26 mwaka huu akiwa na bunduki yenye risasi 29.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki
alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 18 mwaka huu eneo la Kabuku
wilayani saa mbili usiku.
Ndaki alisema
kuwa jinsi ya kukamatwa mtuhumiwa huyo ni baada ya jeshi hilo kupata taarifa za
siri kutoka kwa wasamaria wema kuwa mtuhumiwa huyo alihusika katika unyang’anyi
kwa kutumia silaha katika tukio ambalo lilitokea Januari mwaka huu jijini
Tanga.
Alisema kuwa
baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo walimuhoji na kukiri kuwa alihusika katika
kupora silaha pamoja na kushiriki kwenye tukio hilo pia ni miongoni mwa
majambazi waliokuwa eneo la mapango ya mleni.
Aidha alikiri
pia kuwepo ndani ya pango hilo wakati mapambano baina yao na Jeshi la Polisi na
alikuwa ni mtu wa mwisho kutoka mapangoni humo akiwa na bunduki moja waliokuwa
wameificha ndani humo.
Kaimu kamanda
huyo alisema kuwa Machi 19 mwaka huu baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa saa
mbili asubuhi aliwaongoza askari wa kikosi kazi Taifa wakiwa na Mkuuwa
Upelelezi wa makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga (RCO) kwenda kuwaonyesha silaha
hiyo.
Alisema kuwa
baada ya kufika mapangoni hapo walionyeshwa bunduki moja aina ya SMG yenye
namba 14303545 ikiwa na risasi 29 ikiwa ni miongoni mwa bunduki walizoporwa
askari Januari 26 mwaka huu.
Aidha alisema
kuwa aliwaonyesha panga moja ,Begi moja la kaawia likiwa na nguo mbalimbali na
mabomu matatu ya kutengeneza kienyeji ambazo walikuwa wakivutumia wakati
wakijibizana na askari hao.
Aliongeza
kuwa kupatikana kwa silaha hiyo kunafanya silaha zote mbili walizoporwa askari
wa Jeshi hilo ambao walikuwa doria kupatikana
EmoticonEmoticon