Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza
viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi
ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.
Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi
katika Uwanja wa CCM Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali
ya juu tayari kwa kuwakabili the Flames.
Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili
jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo
la Kirumba,ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa
Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika,
timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja
utakaotumika kwa mchezo.
Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini
Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub,
Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa,
Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma
Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
MALAWI
YAWASILI MWANZA
Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini
Mwanza majira ya saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya
mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji
18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza
soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph
Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji),
Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika
Kusini), Harry Nyirenda (Black Leopards
- Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps
United - Zimbambwe)
Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers),
Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John
Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle),
Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support
Ballaton).
Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young
Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari
wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya
mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi
wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.
Kesho jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi
wa habari katika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa
Stars Mart Nooij na kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi
ya mchezo wao wa siku ya jumapili.

EmoticonEmoticon