Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokelewa na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya alipowasili uwanja wa ndege
wa Sumbawanga kuanza ziara ya kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili eneo la Jangwani mjini
Sumbawanga kuweka jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na
NHC kwa ajili ya kuuzia wananchi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na
Kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya nyanda za juu kusini Bw. Msigwa mara
alipowasili Mkoani Rukwa kutatua migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa msimamo wa
dhati wa serikali (kwa wananchi waliofurika kumsikiliza hawapo pichani)
wenye nia ya kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya mwekezaji na
wananchi wa vijiji vya Skaungu na Mawensuzi alipofika katika eneo la
Malonje Wilayani Sumbawanga.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya
wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwenye nyumba
za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Mkoani Rukwa. Alisisitiza
Halmashauri nchini kutenga ardhi kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za
gharama nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Mchechu akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC
eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi (hayupo pichani) jana.
Mbunge wa Sumbawanga Mhe. Hilal
Aeshi akiishukuru NHC kwa kujenga nyumba za makazi eneo la Jangwani kwa
ajili ya kuuzia wananchi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Skaungu
Bw. Pascal Mwanakatwe akisoma risala kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi kuelezea mgogoro wa
ardhi unaokabili kijiji hicho na mwekezaji kanisa la Efatha baada ya
Waziri Lukuvi kufika eneo la Malonje kuwasikiliza wananchi ili serikali
ipate mwelekeo wa kutatua mgogoro huo.
Watendaji wa sekta ya ardhi
wakiratibu mazungumzo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Vangimembe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa Mkoa wa
Rukwa (hawapo pichani ) juu ya migogoro ya ardhi inayowasumbua wananchi.
Wananchi wa kijiji cha Skaungu
wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William
Vangimembe Lukuvi alipofika kijiji kilichopo kilomita 50 kutoka mjini
Sumbawanga kueleza nia ya serikali ya kumaliza mgogoro wa wananchi na
Kanisa la Efatha ambalo ni mwekezaji na mmiliki wa mashamba
yanayolalamikiwa na wananchi na kukisababisha mauaji ya mara kwa mara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka rasmi jiwe la
msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani
mjini Sumbawanga kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo zinatarajiwa
kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji
Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya ujenzi unaofanyika
eneo la Jangwani kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.
William Vangimembe Lukuvi alipowasili kuweka jiwe la msingi la nyumba
hizo jana.
Kikundi cha ngoma za kifipa
kikiburudisha wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la
msingi nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Sumbawanga
muda mfupi kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.
William Vangimembe Lukuvi kuwasili eneo hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisikiliza na kupokea
barua za malalamiko ya wananchi waliofurika katika ukumbi wa mikutano
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa jana ili kuwasilisha kero zao za
ardhi.
EmoticonEmoticon