Bodi ya Wataalam wa
Ununuzi na Ugavi PSPTB imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya
ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya shahada
ya
Ununuzi na ugavi.
Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe
16 Februari 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha,
ambaye aliwaasa wanafunzi hao wazingatie mafunzo hayo ili kuongeza ubora
wa kazi za utafiti watakazofanya kwa ajili ya kupata shahada ya juu ya
ununuzi na ugavi.
Aidha, alisisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia maadili katika
kufanya utafiti, jambo ambalo ndio msingi na matakwa ya Bodi. wanafunzi
wanatakiwa kufanya utafiti wao wenyewe na sio kuchukua kazi zilizofanywa
na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine maana
kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Pamoja na kuwajengea uwezo wa
kufanya utafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kujiamini, kuandika
ripoti na kujieleza na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za
kazi. Hivyo lengo kuu la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuandika,
kujieleza na kutoa huduma bora kwa taifa, kwani ufaulu wa mwanafunzi,
unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani
huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima
uwezo wake.
Mr.
Godfred Mbanyi, Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akitoa neno katika ufunguzi
wa semina ya utafiti iliyofanyika kwenye ukumbi wa TEC Kurasini Dar es
Salaam tarehe 16/2/2015
Mkurugenzi wa mafunzo Mr.
Godfred Mbanyi akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence
TEsha kufungua semina ya utafiti katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es
Salaam. Tarehe 16/02/2015
Picha
ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB na washiriki wa semina ya
Utafiti iliyofanyika Katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe.
16/2/2015.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence Tesha(aliyeketi katikati), mwezeshaji wa
semina Dr. Eli Tumsifu (aliyeketi kushoto) na Mr. Godfred Mbanyi
Mkurugenzi wa mafunzo (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na
washiriki wa semina
Washiriki
wa Semina ya utafiti wakimsikiliza mwezeshaji Dr. Eli Tumsifu toka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, kwenye semina ya utafiti iliyofanyika katika
ukumbi waTEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16-20 Februari 2015
Dr.
Eli Tumsifu akiwa na washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB ndani ya
ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16-20 Februari 2015
Washiriki
wa semina ya utafiti ya PSPTB wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB
Dr. C. Tesha (aliyeketi katikati), Dr. Eli Tumsifu Mkufunzi wa semina
(aliyeketi kushoto) na Mkurugenzi wa mafunzo wa PSPTB Mr. Godfred Mbanyi
(aliyeketi kulia) wakati wa semina yautafiti iliyofnyika 16-20 Februari
2015 katika Ukumbi wa TEC Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon