Tanzania mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Wahasibu

February 05, 2015

Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu mkutano utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12  mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile jana jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika nchini.
Mhasibu Mkuu wa Serikali Mwanaidi alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Katika mkutano huo, mada mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa zikilenga kwa lengo la kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika masuala ya hesabu za serikali na kutoa fursa ya kuwa na jukwaa kwa ajili ya washiriki ili kufanya tathmini kwa kujadiliana na kushirikishana uzoefu mbali mbali.
Aidha, mkutano huo unalenga kuhamasisha maendeleo ya watendaji wahasibu wa Serikali na kutoa mafunzo stahiki kupitia utekelezaji wa program shirikishi kwa kujifunza uzoefu wa masuala mbali mbali ndani ya nchi wanachama.
Mkutano wa wahasibu hao unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1000 wakiwemo Wahasibu wakuu 14 kutoka nchi wanachama na wadau wengine.
Ujio wa wageni hao pamoja na ushiriki wao katika mkutano wa siku tano utakuwa wa tija na fursa muhimu katika utoaji wa huduma za jamii wakati wote watakapokuwa nchini.
Aidha, katika mahitaji yao ya malazi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi, makadirio ni kwamba kila mgeni anaweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja, hivyo basi kwa hesabu za haraka haraka kutakuwa na matumizi ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano katika muda wa siku tano tu.
“Wito wangu kwa watanzania, nawaomba wajitokeze kushiriki katika mkutano huu wa ESAAG wa 2015, hivyo natoa rai kwa wataalam, wahasibu na wadau wetu wote kwa ujumla wao ili tuweze kushirikiana kuufanikisha mkutano huu wa kimataifa unaofanyika nyumbani, Tanzania” alisema Mwanaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile amesema kuwa nchi washiriki zinazounda umoja huo ni Botswana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
Azizi aliwahakikishia washiriki wote kuwa maandalizi ya mkutano huo katika masuala ya usafiri, usalama na malazi yapo katika hatua nzuri na kamati yake imejipanga vema ili mkutano huo uwe wa mfano wa kuigwa kwa nchi zote wanachama watakapopata fursa ya kuandaa mkutano wa mwaka katika nchi zao.
ni wa serikali wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika,Kwa bahati nzuri chama hiki kikiwa na malengo yafuatayo
ESAAG ni chama cha wahasibu wakuu ambacho kilizaliwa miaka 20 iliypoita Arusha hapa nchini mwaka 1995 na mkutano wa mwaka huu wa 22 wa ESAAG unaongozwa na kauli mbiu “Uimarishaji na usimamizi wa fedha kwa ajili ya Maendeleo ya kijamii na Kiuchumi katika kanda’’.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »