ZIDANE AMPA CASILLAS KIPA BORA DUNIANI, ATAJA KIKOSI CHAKE BORA, YAYA TOURE NDANI

December 18, 2014
ZIDANE (KULIA) AKISALIMIANA NA IKER CASILLAS.
Kocha wa timu ya vijana ya Real Madrid maarufu kama Zizou, amesema tayari kipa Iker Casillas amerejea kwenye ubora wake.

Kiungo huyo nyota wa zamani wa Real Madrid amesema Casillas amerudi katika kiwango chake cha juu.

Ingawa kipa wa Bayern Munich na Ujerumani Manuel Neuer ndiye anaonekana bora hadi kuingia kuwania FIFA Ballon d'Or  2014 akiwa na Cristiano Ronaldo na  Leo Messi, mkongwe huyo amesisitiza, Casillas sasa amerudi kwenye nafasi yake.

Akihojiwa na runinga ya Canal Plus ya Ufaransa, Zidane alisisitiza, Casillas ndiye kipa bora zaidi duniani kwa kipindi cha miaka kumi.

Wachezaji wengine aliowasifia ambao wanacheza katika kiwango cha juu ni mabeki wa Madrid, Sergio Ramos, Pepe na Marcelo pamoja na Dani Alves kutoka Barcelona.

Kwa upande wa kiungo, Zidane ameweka wazi kwamba anavutiwa na Mwafrika kutoka Ivory Coast, Yaya Touré anayekipiga Man City, pia Luka Modric wa Madrid kutokea Croatia.


Kwa upande wa washambuliaji, amewataja wanne ambao anaamini ni bora kuwa ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na Karim Benzema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »