POLISI TANGA YAFANIKIWA KUOKOA NYAYA ZA UMEME ZENYE THAMANI YA SH.MILIONI 7 ZILIZOKUWA ZIMEFICHWA

December 18, 2014

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kuokoa nyaya za umeme zenye thamani ya sh milioni 7 zilizokuwa zimefichwa porini kwenye Kijiji cha Magoma wilayani Korogwe ambazo zilikuwa kwenye mchakato wa kusafirishwa kwa ajili ya kuziuza kwenye maeneo mengine.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki ameimbia Tanga Raha Blog Ofisi kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi ambapo nyaya hizo ziliibiwa na watu wasiofahamika na kwenda kuzihifadhi kwenye eneo hilo ambazo zilionekana .

Alisema kuwa ugunduzi wa nyaya hizo uligunduliwa na Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Suleimani Kalulu mkazi wa Kwamkole ambaye alibaini kuwepo kwa kasora ya waya wenye urefu wa mita 1080 ambazo zilikuwa zimeibiwa.
 
Kaimu Kamanda huyo alisema baada ya kugundua kasoro hiyo walianza msako wakishirikiana na askari ndipo walipobaini zilikuwa zimefuchwa porini .

Aidha alisema kutokana na tukio hilo hakuna mtu yoyote ambaye anashikiliwa Jeshi hilo wakati askari wakiendelea na msako mkali ili kuweza kuwabaini wahusika wake ili waweze kuchukulia hatua.

  “Kama ujavyojua sisi tulipata taarifa hizo na tunajipanga vilivyo kuhakikisha tunafanikisha kupatikana na kwa bahati nzuri kwenye msako wetu tulifanikiwa kuzikuta zimetelekeza porini “Alisema Kaimu Kamanda Ndaki.
 
Hata hivyo,Kaimu Kamanda Ndaki aliwataka wananchi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapowabaini wezi wa miundombinu ya umeme ikiwemo nyaya ambazo hupelekea kuliingiza shirika hilo kwenye hasara ili waweze kuchukua hatua .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »