WAKAGUZI WA MIGODI WAPIGWA MSASA

December 15, 2014
unnamed
Baadhi ya Wakaguzi wa Madini kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi kuandaa miongozo (checklist) ili itakayosaidia katika kutekeleza shughuli za ukaguzi wa migodi.
unnamed1
Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje (katikati) akiongea jambo wakati akifungua rasmi kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini , Uratibu, Mhandisi John Shija, kulia ni Mhandisi Laurian Rwebembera.
unnamed2
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.
unnamed3
Mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Chagwa Marwa, (kushoto) akichangia jambo wako wa majadiliano ya kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi. Anayesikiliza ni Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Assa Mwakilembe.
…………………………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Mwanza
Wakaguzi wa Migodi kutoka mikoa mbalimbali nchini wamekutana katika kikao kazi kwa lengo la kuandaa miongozo (checklist) itakayo wawezesha kutekeleza kikamilifu majukumu yao wawapo katika shughuli za ukaguzi wa migodi.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje amewataka wakaguzi hao kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kufanyika kwa ukaguzi yakinifu ili kuwezesha usalama migodini.
Mhandisi Samaje ameongeza kuwa, wakaguzi wa migodi wanao wajibu kuhakikisha usalama na afya migodini na kuongeza kuwa, masuala ya uhifadhi wa mazingira pia ni jambo la kuzingatia wakati wa kufanya ukaguzi.
“Naomba tuwe makini katika kutoa maoni yatakayosaidia kuandaa ‘checklist’, tumieni uzoefu mlionao tuboreshe jambo hili, ongezeni masuala mapya ambayo yatakuwa na manufaa katika shughuli za ukaguzi wa migodi. Lazima tutofautishe kutembelea na kukagua migodi,” ameongeza Samaje.
Aidha, amewataka kuwa makini na kutekeleza shughuli hizo kitaalamu kutokana na umuhimu wake na kuongeza, “tukikutuma kufanya ukaguzi, tunataka uende kama mtaalamu kweli unayefahamu majukumu yake. Kwa hiyo, maoni mtakayotoa leo, yatakua na mchango mkubwa katika shughuli za ukaguzi,” amesisitiza Samaje.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa zikilenga kuwajengea uwezo wa namna bora ya kufanya shughuli za ukaguzi migodini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »