Benki ya NBC yawapiga jeki vijana na kuwakumbuka yatima

December 15, 2014


Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) akitoa elimu kuhusu ujasiriamali na baadhi ya vijana kutoka vyuoni walio katika kambi maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Maa Media kwa udhamini wa NBC mjini Bagamoyo, Pwani hivi karibuni. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 ambapo mbali na ujasiriamali vijana hao walifundishwa pia madhara na jinsi ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kulia), akisalimiana na Meneja Miradi wa Kampuni ya Maa Media, Albany James wakati yeye na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (kulia) walipotembelea kambi ya vijana iliyoandaliwa na Maa Media ili kuwafundisha masuala ya ujasiriamali, madhara na jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 kwa ajili ya kambi hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lekoko Furaha.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda akifanya mahojiano na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe.
Vijana wakijiweka sawa kabla ya kuanza kwa mafunzo yao.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari wakati uongozi wa benki hiyo ukitembelea kambi ya vijana iliyoaandaliwa na Maa Media kwa udhamini wa benki ya NBC.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »