Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo
wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya
Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Lazaro Nyalandu akiagana na mzee wa kimasai mara baada ya kumaliza
mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa jamii
ya Wamasai katika eneo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii
ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki).
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa
jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza mkutano nao.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia
tamko la serikali juu ya uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai
katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika kisima kilichojengwa kwa
ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika eneo la Loliondo.
………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka
kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro
mkoani Arusha hazina ukweli wowote.
Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza,
liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai
wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro
mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote
isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na
wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya
Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,”
alisema.
EmoticonEmoticon