MAJAMBAZI
wawili wamefariki dunia na wengine kukimbia kusikojulikana kwa kupata kipigo
kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya jaribio la kupora mishahara ya wafanyakazi katika kiwanda
cha Chokaa cha Meelkh Limietd kilichopo Amboni Jijini Tanga kushindikana.
Tukio hilo
lilitokea Novemba 7 mwaka huu majira ya saa saba na nusu mchana ambapo majambazi hao walifika
kiwandani hapo kwa lengo la kuporwa fedha hizo ambazo walishindwa kuzipata
katika jaribio.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki(Pichani Juu aliyesimama) alisema kuwa tukio hilo litokea Mtaa
wa Amboni Kata ya Amboni Tarafa ya Mzizima ambapo majambazi hao walikwenda wakitumia
usafiri wa pikipiki yenye namba za usajili MC36ABE aina ya Honda.
Aliwataja
majambazi waliouwawa kuwa ni Timoth Charles(36) mkazi wa Mkwajuni jijini Dar es
Salaam pamoja na Mwinyimkuu Hamisi(46) mkazi wa Chanika Jijini Dar es Salaam
ambapo walifariki dunia wakiwa njiani wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu.
Alisema
kuwa katika tukio majambazi wenzao walifanikiwa kukimbia na kutokomea
kusikujulikana wakati msako mkali ukiendelea ili kuweza kuwabaini waliokimbia
kuweza kuchukuliwa hatua.
Hata hivyo
Kaimu Kamanda huyo alitoa wito kwa kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria
mikononi kwa kuwauwa wanzao ambao wanadhaniwa kuwa ni wahalifu wa makosa
mbalimbali ikiwemo ujambazi badala yake wawakamate na kuwafikisha kwenye vyombo
vya kisheria.
“Huo sio utaratibu mzuri wa kujichukulia
sheria mikononi kwa kuwaadhibu waahalifu ni vema mnapowakamata mkawapeleka
kwenye vyombo ya sheria ili waweze kuchukua hatua kuliko kufanya hivyo “Alisema
Kaimu Kamanda Ndaki.
Katika
hatua nyengine aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwenye maeneo
yao ili kuweza kudumisha hali ya amani na usalama iliyopo hapa nchin.
EmoticonEmoticon