Mwandishi wetu,Arusha
WIZARA
ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni
(PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia
thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri
watu wasio na sifa kufanya kazi hizo
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua
mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la
Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia
maadili na miiko ya kazi yao.
Amesema
katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni
20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya
bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee
katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya
mkutano huo “Thamani halisi ya fedha za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha
serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua
uchumi wa nchi.
Amesema
Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali
ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri
watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa Bodi ya Wataalamu wa
Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa Siku mbili unaofanyika kwenye
kituo cha mikutano cha AICC, jijini Arusha.
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa Siku
mbili wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) unaofanyika
kwenye kituo cha mikutano cha AICC jijini Arusha.
Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence
Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba
nzuri.
Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha
EmoticonEmoticon