Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiteta na
wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na
Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika pozi
na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na
Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika picha
ya pamoja na walemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mafunzo ya usajisiriamali
kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini.
*************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred
Foundation (BAF) imeendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 50 wenye ulemavu
wa ngozi.
Brigitte aliendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na
taasisi ya Junior Achievement Tanzania yalifungwa jana kwenye viwanja vya
Makumbusho ya Taifa na kupambwa na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali
mbalimbali ambao ni zao la mradi huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Brigitte alisema kuwa
mafunzo hayo yamelenga mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku ikiwa pamoja
na kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.
Alisema kuwa BAF kupitia Taasisi ya Junior Achievement
Tanzania kwa pamoja wameweza kutoa elimu ya kujitambua na stadi za biashara ili
walemavu wa ngozi waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na
shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa
maisha yao na familia zao.
Alisema kuwa mpango huu umekuwa wa kipekee kwa kundi
hili kwa kuweza kuwajengea mtazamo chanya wakuthubutu, kujiamini na kuweza
kufanya mambo makubwa katika maisha.
“Mpango huu umeanza
hapa Dar es Salaam, ila Brigitte
Alfred Foundation ina azma ya kuuendeleza nje ya Dar es Salaam na kufikia
walengwa waliopo mikoa tofauti nchini kwa sababu umeleta manufaa na mabadiliko
makubwa sana kwa hawa vijana wenye ulemavu wa ngozi katika muda mdogo na
umeonyesha kwamba walemavu wakiwezewshwa,” alisema Brigitte.
Mrembo huyo alitoa shukrani kwa Juniour Achievement Tanzania na wadhamini
wakuu, kampuni ya Azam kwa kutoa mafunzo hayo ambayo anaamini
wahitimu watayatumia kwa faida zaidi.
“Nawaomba wadau wengine waniunge mkono katika mpango
huu kwani awamu inayofuata ambayo ni kutekeleza mipango yao ya biashara katika
ujasiriamali ili kuendeleza vijana wetu wa Tanzania hususa walemavu ili weweze
kujikimu na kuboresha maisha yao kwa ujumla,” alisema.
EmoticonEmoticon