Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Seif Rashid akifungua Kongamano la
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wahariri pamoja na waandishi wa habari
wa vyombo mbalimbali linalofanyika kwenye hoteli ya New Dodoma mkoani
Dodoma jana, Kongamano hilo la siku mbili linaendelea leo na linajadili
mafanikio mbalimbali na changamoto zinazokabili mfuko huo katika mikoa
mbalimbali na Halmashauri ambazo unatoa huduma zake. Kongamano hilo
linamalizika leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA)
Naibu
Katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr.
Deo Mtasiwa akizungumza katika kongamano hilo wakati akimkaribisha
waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid ili kuzungumza na
washiriki wa kongamano hilo.
Kamimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Khamis Mdee akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Athman Rehani wakiwa katika mkutano huo.
Hance John Mwankenja Afisa Mwandamizi , Matekelezo NHIF pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Elibariki Kingu akitoa mada katika kongamano hilo. Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Bw. Athman Rehani akitoa mada katika Kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Said Ally wakiwa katika kongamano hilo.
Hosea Cheyo wa TBC Mbeya kushoto na Tom Chilala wa Star TV wakifuatilia mada. Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Baadhi ya maofisa wa NHIF wakiandika mambo muhimu katika kongamano hilo.
EmoticonEmoticon