SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LASHAURIWA KUHUSU UFADHILI LIGI DARAJA LA KWANZA NCHINI.

October 17, 2014
SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limeshauriwa kuangalia namna ya kuzitafutia ufadhili timu zinazoshiriki michuano ya Ligi daraja la kwanza nchini ili kuweza kuongeza ushindani na ladha ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa ligi kuu soka Tanzania.
Hatua hiyo inatokana na timu nyingi zinazoshiriki ligi hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha jambo ambalo linapunguza ushindani na kuzifanya timu zinazojiweza kucheza vema na kuweza kufikia malengo waliojiwekea.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Kocha Mkuu wa timu ya African Lyon Charles Ottieno mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya African Sports ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha bao 1-0,mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini hapa.
Katika mchezo huo bao la African Sports liliwekwa wavuni na Hassani Materema kunako dakika ya 10 baada ya kumalizia kazi nzuri iliyokuwa imefanywa na Ayoub Masoud ambapo bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliingia uwanjani hapo ikiwa na lengo la kutaka kupanda ushindi ambapo African Lyon walionekana kubadilika na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao bila mafanikio ya aina yoyote yale.
Naye kwa upande wake,Kocha wa African Sports,Ally Maliki alisema wanamshukuru mungu kwa kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi hiyo na kuhaidi kujipanga vema ili kufanya vizuri kwenye michezo yao iliyosalia lengo likiwa kuipandisha timu hiyo kucheza Ligi kuu msimu ujao.
Kwenye mechi hiyo kikosi cha African Sports kiliwakilishwa na Yusuph Yusuph,Ayoub Masoud,Issa Shabani,Juma Shemvuni,Mwaita Ngereza,Hussein Issa,Evarigestus Munjwahuka,Daudi Milandu,Hassani Materema,Ally Ramadhani na James Mendy.
Kwa upande wa African Lyon wao waliwakilishwa na Abubakari Hashim,Omari Kindamba,Kassim Simbaulanga,Baraka Jaffari,Yusuph Mlipili,Hamadi Manzi,Miraji Athuman,John Simbeta,Omary Ramadhani,Kashakala Ndere na Abdallah Mguihi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »