SARE YA LIPULI YAIPASUA KICHWA AFRICAN SPORTS

October 17, 2014


KIKOSI CHA TIMU YA AFRICAN SPORTS .
Kitendo cha timu ya African Sports “Wanakimanumanu” kuruhusu sare na timu ya Lipuli ya Iringa kwenye mechi ya Ligi daraja la kwanza uliochezwa jana kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jambo hilo limewaumiza viongozi wa timu hiyo na kuifikia hatua ya kuwaweka kitimito wachezaji wao.
Kitimoto cha wachezaji hao waliwekwa mara baada ya kumalizika mechi hiyo kwenye uwanja wa huo ambapo wachezaji wote walikalishwa na viongozi wao na kupewa mawaida ya kuhakikisha hawaruhusu sare nyengine mechi inayofuata.
Mechi hiyo ilimalizika kwa timu zote kutoka sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika tisini za mchezo huo ambapo African Sports ndio walikuwa wakwanza kupata bao lao kupitia Ally Ramadhani dakika ya 44 kwa njia ya penati iliyotokana na mchezaji wa timu hiyo Hassani Materema kufanyiwa madhambi na Stone Peter wa Lipuli eneo la hatari na mwamuzi wa mechi hiyo Klina Kabala kutoka Dar kuamuru ipigwe penati.
KIKOSI CHA LIPULI FC YA IRINGA.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zikienda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliingia uwanjani hapo ikiwa na hari mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji
wao.
Lipuli FC ndio walikuwa wa kwanza kuweza kufanya mabadilio ambapo walimtoa Keneth Kipanga na kumuingia Lawama Onole wakati African Sports iliwatoa Hussein Issa na Evarigestus Munjwahuki ambao nafasi zao zilichukuliwa na Maulidi Abbasi na James Mendy.

Akizungumza mara baada ya kumalizika mechi hiyo,Kocha wa African Sports,Ally Manyani alisema kuwa kubwa lililopo mbele yake ni kuhakikisha wanayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo ili waweze kupata ushindi.

Aidha aliwataka wadau wa soka kuendelea kuisapoti timu hiyo ili iweza kutimiza malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanapata nafasi ya kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »