ZAIDI ya kg 2000 za
madawa ya kulevya aina ya Bangi yameteketezwa chini ya Usimamizi wa Jaji wa Mahakama kuu
Kanda ya Tanga,Upendo Msuya wakiwemo viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Tanga.
Utekelezaji huyo
ulifanyika jana kwenye dampo la Duga lililopo Kata ya Duga jijini Tanga ambapo
magunia ya dawa za kulevya yapatayo 48 yaliyokamatwa kwenye matukio mbalimbali
mkoani hapa yalitekelezwa baada ya kesi za watuhumiwa hao kufanyika.
Akizungumza katika
utekelezaji huo,Jaji Msuya alisema gunia hizo 48 zilikamatwa kuanzia mwaka 2009
-2013 ndio yaliyotekelezwa kwa awamu ya kwanza ya amri ya mahakama kuu na
yaliyotekelezwa kwa awamu ya pili ni amri ya mahakama ambayo ni magunia 14
iliyotolewa na Jaji Msuya.
Alisema kuwa watuhumiwa
wa kesi hizo walipatiwa hukumu na walikiwsha kutekeleza vifungo mbalimbali
gerezani na wengine walilipa faini ya kati ya milioni 4 hadi 5.
Aidha alisema kuwa
watuhumiwa waliokamatwa kutokana mwaka 2011 walikuwa na 10 waliokuwa
wametumikia vifungo wakiwemo madereva wa magari na wasafirishaji.
Awali akizungumza mara
baada ya tukio hilo,Ofisa Upelekezi Mkoa wa Tanga (RCO),Aziz Kimatta alisema
utumiaji wa dawa hayo una madhara makubwa sana kwa binadamu na hivyo kuwataka
viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa
elimu kwa waumini wao ili kuweza kutokomeza hali hiyo kwenye jamii.
“Kimsingi ili kuweza kutokomeza hali hii
lazima jamii itambue kuwa dawa hizo zina athari kubwa sana kwao pamoja na
viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu kupitia mawaidha mbalimbali madhara
yake ili kuwabadili kuacha kutumia madawa hayo “Alisema RCO Kimatta.
EmoticonEmoticon