Arjen Robben anapanga kujenga nyumba ya makumbusho
WANASOKA wengi wanafanikiwa kutunza vitu vichache kati ya vingi walivyoshinda katika maisha yao ya soka.
Lakini nyota wa Bayern Munich, Arjen Robben amekuwa na wazo la kutunza kila kitu alichofanikiwa kushinda.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Chelsea na PSV Eindhoven ametangaza
kuwa ana mpango wa kujenga nyumba ndogo ya makumbusho na kutunza vitu
vyote alivyoshinda kama ishara ya kumkumbuka akimaliza maisha yake.
"Nikiwa nimekaa na mke wangu ndani,
niliota kukusanya vitu vyote na kujenga nyumba binafsi ya makumbusho.
Itakuwa kwa ajili yangu, familia yangu na marafiki zangu wa karibu,"
nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliwaambia Bild.
Mholanzi huyu anahakikisha kuwa kila alichoshinda hakisahauliki
Robben alishinda La Liga na kombe la ligi la Hispania wakati huo akicheza Real Madrid
"Nina vitu vingi-zikiwemo jezi za
wachezaji wengine. Nimetunza mpira kutoka fainali ya ligi ya mabingwa
2013 (Bayern ikiifunga Borussia Dortmund 2-1 na Robben alifunga goli la
ushindi dakika za majeruhi).
"Kuna viatu nilivyoshinda katika
michuano ya ubingwa ulaya na kombe la dunia. Wazo ni kuvikusanya pamoja
ili kisipotee hata kimoja".
EmoticonEmoticon