KATIBU SEFUE AWAPA SOMO WATUMISHI WA HALMASHAURI MKOANI TANGA.

September 17, 2014
                      









                        NA MWANDISHI WETU,TANGA.
KATIBU MKUU Kiongozi Balozi,Ombeni Sefue amewaonya watumishi wa serikali wenye tabia ya kudanyanga katika masuala mbalimbali yakiwemo ya malipo madai yao kwa kuwataka kuacha mara
moja kwani watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Sefue alitoa wito huo wakati wa mkutano wake na watumishi wa sekretarieti ya mkoa na taasisi za serikali mkoani Tanga ambapo alisema kuwa wapo baadhi ya watumishi ambao wanafanya udanganyifu baada ya kulipwa madai yao na baadae kudai tena jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa .

Amesema mara nyingi watumishi hao wamekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa kuidanganya serikali kwa kutaka kulipwa madai ambayo tayari yalikwisha kulipwa na mamlaka husika hivyo kabla wao hawajafanya hivyo watashughulikiwa ili kuweza kukomesha tabia hiyo.

  “Tunashangaa sana tabia za baadhi ta watumishi ambao sio waaminifu hasa katika masuala ya malipo kwa kudai mara mbili licha ya kulipwa hivyo nataka niwaambie acheni mara moja jambo hilo kwani mtakaobainika mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo “Alisema Sefue.

Akizungumzia suala la watumishi wa serikali kujiingiza katika masuala ya siasa,Sefue alisema watumishi wa kada hizo hawapaswi kufanya hivyo ikiwemo kuwaonya kuacha kufanya hivyo mara moja kwa sababu watakuwa wamekiuka taratibu zilizopo kisheria.

Badala yake aliwataka wafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na serikali iliyopo madarakani lengo likiwa kuharakisha kasi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini .

  “Kama kuna watumishi wa serikali wanataka kujiingiza kwenye siasa ni bora wakachagua moja waache kazi na kuendelea siasa kwa kufuata taratibu zilizopo kisheria kwa sababu hawawezi kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja “Alisema Katibu Kiongozi.

Alisema jambo hilo linasababisha wakati mwengine kuchukua muda mrefu kujiridhisha ili kuweza kujua madai yaliyopo yaweze kulipwa badala ya kupokea madai na kulipa kwa wakati kutokana na vitendo vya baadhi yao kufanya udanyanyifu kutokana na kutaka kulipwa madai mara mbilimbili.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »