Kikosi
cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari kuelekea
jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania
bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT,
septemba 20 mwaka huu.
Kocha
msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya
wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na viongozi watano kwenda
kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.
Viongozi wa Kagera Sugar
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.
Baadhi
ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba
wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu
Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20
mwaka huu.
Kikosi cha Kagera Sugar
Murage
Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa
mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia
marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga..JPG)
Kocha
Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake
wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi
karibuni.
EmoticonEmoticon