Wanandinga wa Coastal Union (Jezi
nyekundu) wakisalimiana na wachezaji wa timu mpya ya ligi kuu soka
Tanzania bara, Polisi Morogoro katika mechi ya kirafiki iliyofanyika
mwishoni mwa wiki katika tamasha la 'Coastal Union Day' septemba 7
mwaka huu uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ambao Wagosi wa Kaya
walishinda 2-0.
Wachezaji wa Coastal Union wakiongozwa na mlinda mlango maarufu, Shaban Hassan Kado (Jezi namba 30) kuomba dua kabla ya mechi
Kikosi cha kazi cha Coastal Union
Mashabiki wa soka Jijini Tanga
walifurika kwa wingi kuitazama timu yao iliyoweka kambi ya mwezi mmoja
kisiwani Pemba kujiwinda na michuano mipya ya ligi kuu soka Tanzania
bara na itaanza kampeni zake kwa kuchuana na Simba uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam, septemba 21
Hapa vijana wa Coastal Union chini ya kocha Mkenya, Yusuf Chipo walikuwa wanapasha moto misuli kabla ya kuanza mechi
EmoticonEmoticon